Masharti ya matumizi

Imewekwa: Oktoba 2026.

Kazi ni mali ya waandishi wake

Kila kazi iliyoko kwenye Wazo (mashairi, tungo, makala, stori na vitabu) ni mali ya mwandishi wake, kama inavyoonyeshwa chini ya kazi hiyo. Wazo inaonyesha kazi hizi kwa ruhusa ya waandishi wake.

Waandishi wanawajibika kwa kazi zao

Kila mwandishi anathibitisha kwamba kazi anayoleta Wazo ni yake mwenyewe, au ana ruhusa ya kuitumia. Wazo haiwajibiki kwa kazi ambayo mwandishi ameichukua kwa mtu mwingine bila ruhusa.

Unachoweza kufanya kama msomaji

Unaweza kusoma bure, kushiriki viungo vya kazi, na kunukuu sehemu fupi ukimtaja mwandishi na kuweka kiungo cha Wazo. Huruhusiwi kunakili kazi nzima, kuichapisha mahali pengine, au kuiuza bila ruhusa ya mwandishi.

Ukiona kazi iliyochukuliwa bila ruhusa

Kama unaamini kazi fulani kwenye Wazo ni yako au imechukuliwa bila ruhusa, tuandikie kupitia ukurasa wa Wasiliana: weka kiungo cha kazi hiyo na maelezo mafupi. Wazo itaificha kazi hiyo wakati inachunguza, na itaiondoa kabisa kama itathibitika imechukuliwa bila ruhusa.

Mabadiliko

Masharti haya yanaweza kubadilika. Tarehe iliyo juu inaonyesha mara ya mwisho yalipobadilishwa.