Usipoteze Maisha Yako
Kuna kitu ambacho hakuna mtu yeyote amewahi kukuambia au kukushauri kuhusu maisha; sio shuleni, si wazazi wako, wala sio hata kwenye vitabu wanavyosema kuwa ukivisoma vitakupa majibu ya maswali yako.
Lakini unajikuta tu umejifunza kwa njia ngumu! Baada ya miaka mingi ya kukwama, au kupoteza uelekeo, au baada ya kuhisi labda huenda kuna jambo halipo sawa.
Kwa kipindi kirefu nimejikuta kama nipo nje ya mfumo hivi, nikiwa nayaangalia maisha kama filamu ya kuigiza, hadi nikaona kwamba "HUENDA KUNA NJIA YA SIRI KWENYE MAFANIKIO YA KILA UNAYEMFAHAMU". Kabla ya kugundua hili nilikuwa nikiishi maisha ya kujiburuza tu.
Kila usiku nilikuwa nikijiuliza kwamba; Kwanini mpaka sasa sijafikia mafanikio ninayoyahitaji? Mbona najiona nipo nyuma sana? Ni sehemu gani hasa sifanyi kwa ufanisi?
Na ghafla siku moja kuna kitu nikagundua, na baada ya kugundua; mambo mengi yakaanza kubadilika kwenye maisha yangu. Kilichonigharimu takribani miaka kumi kujifunza naweza nikakuelekeza kwa dakika chache tu kupitia kitabu hiki kidogo.
Na ukielewa hii, nakuhakikishia kuwa maisha yako hayatabaki kama ulivyo.
Watu wengi wamejikuta wanakwama kwa kutegemea kusubiri hadi waone wameshapata kila kitu ndiyo waanze utekelezaji wa mipango yao, wanajiambia "nitaanza nikiwa tayari, nahitaji kujiandaa kwanza! Au nisubiri muda sahihi wa kuanza!" Sasa huu ni ukweli mchungu; KUSUBIRI NI UDANGANYIFU.
Ukisema USUBIRI ni mtego tu huo, kwa kadiri unavyosubiri, ndiyo inakuwa ngumu zaidi kufanya maamuzi ya KUANZA. Unaweza kuamua KUSUBIRI kwa siku moja, unajikuta imefika wiki, na baadae hata mwaka mzima, na kabla hujaelewa vizuri, unakuta tayari ni miaka 10 imepita. Na wewe bado unasubiri tu!
Na hivyo, hivyo ndiyo watu wengi wanayapoteza maisha yao. Wanabaki wamekaa tu wakiyaangalia maisha yanasonga mbele badala ya kuishi katika uhalisia wao.
Jaribu kufikiria, ni mara ngapi umejiambia nitaanza kesho, ni ndoto ngapi umezipoteza kwasababu ulijiona bado hujawa tayari kuanza? Ukweli ni kwamba kamwe hutakuja kuona upo tayari! Na huo ndiyo ukweli, kwasababu maisha hayahusiani tu na mwamzo uliokamilika unaouhitaji, ni kuhusu kuanza kutengeneza unachotaka, bila kujali hali uliyonayo kwa sasa.
Sasa unawezaje kuacha kusubiri, na kuanza kusonga mbele? Inaanza na mgawanyiko wa hatua 3. Baada ya kuelewa hii, hutabaki kama ulivyo.
Hakuna yoyote anayekuja kukusaidia
Hakuna yeyote anayekuja; si wazazi, au marafiki, wala hata bosi wako. Hakuna yeyote mwenye jukumu la kuboresha maisha yako isipokuwa wewe tu. Ukishaelewa hii utaacha kusubiri, utaachana na matarajio ya kusubiri muda sahihi, na utaamua kuwajibika. Ukigundua maisha yako yanakutegemea wewe kwa asilimia miamoja, hutakuwa na muda wa kusubiri.
Maamuzi yanatengeneza muendelezo
Watu wengi wanashindwa kufanya maamuzi, wanataka hadi wapate hisia za kuanza. Wanahisi labda huenda kunaweza kuwa na muujiza unaweza kuwasaidia kufanya maamuzi, au wakakutana tun a bahati. Ukisema utasubiri tu muujiza ni kama kumtegemea mtu mwenye mipango mizuri halafu linapokuja suala la utktlezaji humuoni akiitekeleza. Ni lazima ufanye maamuzi ya kuanza bila kuogopa hali uliyonayo, na muujiza, au bahati utakukuta mbele ya safari. Kwahiyo chochote unachotaka kufanya, usisubiri hadi ujione umekamilika! Anza sasa.
Tumia sekunde tatu
Unaweza kuwa umepata wazo, au kuna jambo unataka kufanya, sasa ubongo huwa unajitengenezea maswali kama haya (Vipi kama sitafanikiwa? Au watu watanionaje? Vipi kama sina mtaji wa kutosha?) Hii ndiyo namna ya kufanya kwa sekunde tatu; tumia sekunde tatu. Chochote unchotakiwa kukifanya kwaajili ya kuboresha maisha yako, hesabu hadi tatu (1, 2, 3) fanya maamuzi! Unataka kupiga simu-piga, unataka kutuma sms-tuma, unataka kufanya usafi-fanya. Ila ukisema usubiri kidogo utajikuta unaendelea kupata sababu za kuendelea kusubiri tu.
“Leave nothing for tomorrow which can be done today” - Unknown