Sera ya faragha

Imewekwa: Oktoba 2026.

1. Taarifa tunazokusanya

Ukisoma bila kuingia, Wazo haikusanyi taarifa zako binafsi, kama jina au barua pepe.

Ukiingia kwa Google, Wazo inapokea barua pepe yako tu. Haipati nenosiri lako wala taarifa nyingine za akaunti yako ya Google.

2. Jina lako

Jina unalochagua linaonekana kwa wengine pale tu unapochapisha kazi zako. Barua pepe yako haionyeshwi kwa mtu yeyote.

3. Tunavyotumia taarifa

Taarifa zinazotokana na matumizi yako ya Wazo zinabaki ndani ya Wazo, na zinatumika tu kukupa huduma bora na kurahisisha matumizi yako.

4. Hatushiriki taarifa zako

Wazo haiuzi wala haishiriki taarifa zako na mtu yeyote, na haitumii matangazo wala huduma za kufuatilia za makampuni mengine.

5. Kufuta akaunti yako

Unaweza kufuta akaunti yako wakati wowote kwenye ukurasa wa akaunti yako. Taarifa zako zote za account yako zitafutwa pamoja.

6. Maswali

Maswali kuhusu taarifa zako: tumia ukurasa wa Wasiliana.